Breaking News: Moto mkubwa waunguza Soko Mbagala
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii Machi 6, 2018.
Sehemu iliyoathirika zaidi ni ile ya wauza mitumba huku baadhi ya bidhaa zao zikiteketea kwa moto lakini hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa.
Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo tayari gari la jeshi la zima moto limefika kuzima moto huo.
MOTO WAUNGUZA SOKO MBAGALA
Reviewed by taragwa
on
March 05, 2018
Rating:
Reviewed by taragwa
on
March 05, 2018
Rating:


No comments: