Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, ametajwa kucheza mchezo
ujao wa Kombe la Shirikisho ambao Simba wataikabili Al Masry SC ya
Sudan, Jumatano ya wiki lijalo.
Okwi ambaye aliumia katika mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC na kupelekea
kutolewa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na Laudit Mavugo, hali yake
kwa sasa inaendelea vizuri na kufikia Jumatano atakuwa fiti kucheza.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema Okwi atacheza mchezo huo.
Mbali na Okwi, Manara amesema pia, mshambuliaji wao aliyeumia kwenye
mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC, John Bocco, atakuwepo katika mchezo
huo wa Kombe la Shirikisho kutokana na hali yake kuendelea vema hivi.
Bocco amekosekana katika mechi zaidi ya mbili ambazo ni dhidi ya Mbao FC
na Stand United, pia Gendarmarie Nationale FC kutokana na majeruhi.
Ujio wa wachezaji hao ndani ya Simba unaweza kuleta manufaa kutokana na
namna ambavyo wamekuwa wakiihimili safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi
chao.
Okwi vs Bocco wapo fiti 1%
Reviewed by taragwa
on
March 03, 2018
Rating: 5
No comments: